Habari

Kunyoa au kuacha

Siku moja nilikua katika saluni moja Mikocheni nikizitengeneza nywele zangu, (kuziosha na kukausha tu kwa hewa ya moto) tena nilikuwa na shoga yangu ambaye alikuwa anasukwa nywele. Dada aliyekuwa anamsuka alikuwa amevaa pentsi za zilizopita magoti yake kidogo na nilivutiwa na miguu yake. Miguu hiyo ingeweza kuwa ya mwanaume kwa urahisi. Ilikuwa ina malaika nyingi ni dhahiri kuwa alikuwa hajawaji kunyoa hata siku moja!
Lakini hii haikuwa mara yangu ya kwanza kumwona mwanamke ambaye hakunyoa miguu au makwapa hapa Tanzania, kwa hiyo niliaanza kulitafakari swala hili liitwalo kunyoa. Kwanini wanawake hujinyoa? Desturi hii ilianza wapi? Je, ni desturi ya kitamaduni katika jamii nyingi?

Kufuatana na makala moja iliyoandikwa na Christine Hope mnamo 1982 katika gazeti la “Journal of American Culture”, tabia ya kunyoa ilianza huko Marekani, kufuatana na makala yaliyoandikwa kwa jina sahihi kabisa “Malaika wa Mwili wa Mwanamke Mkaukazi na Utamaduni wa Kimarekani” Mtindo wa mavazi ya kike yasiyo na mikono yalipoanza kuvuma, wimbi la matangazo na mabango lilionesha wasichana wenye makwapa yaliyonyolewa laini na misamiati isemayo hivi, “Mavazi ya Kiangazi na Dansi za Kisasa huunganika kulazimisha uondoaji wa nywele au malaika zinazochukiza.”

Kampeni hii dhidi ya mafuzi ya kwapani ilianza mnamo mwaka 1915, na iliongezeka kadri mtindo ulivyoendelea kukua. Kadri magauni na sketi vilivyozidi kuwa fupi na nguo za kuogelea zikawa zinabaini zaidi mwili, unyoaji ukawa jambo linalofaa na dexturi inayokubalika kijamii katika jamii za magharibi.

Desturi ya unyoaji miguu sasa inatumika sana katika nchi za Brazil, Amerika ya Kaskazini, Mashariki ya Kati, India, na Ulaya; ingawa wanawake wa Ugiriki na jimbo la bahari ya Mediteranean hawanyowi kabisa, wakipendelea kubaki na uasilia wao. Baadhi ya wanawake huamini kuwa unyoaji ni uchafuzi wa mazingira kwa sababu ya utupaji wa nyembe ya kunyolea, na wengine hawajali kabisa!

Kwa hiyo unyoaji una faida gani? Kufuata na maoni ya mabingwa wa ngozi, baadhi ya faida za unyoaji ni kama ifuatavyo , hupunguza kasi ya kupata makunjo usoni, kuondoa chembe za ngozi zinazokufa, hurudisha ujana katika ngozi, hasafisha, na kuondoa kuwashwa kunaoletwa na nywele au malaika za usoni.

Kwa hiyo kunyoa au kuacha naamini kabisa kuwa suala la uamuzi wa mtu binafsi. Inakubidi kujiuliza jambo linalokufurahisha zaidi ni lipi? Kama jibu lako ni kutupilia mbali wembe wako na kuhifadhi kile ulichopewa na mama yako, basi fanya hivyo bila shaka.

Na kama uamuzi wako utakufanya uelekee kwa duka la dawa au duka lolote lililo jirani kununua paketi ya wembe au dawa ya kuondoa nywele ili upate kuonekana laini na mororo, basi usisite, nenda tu!

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents