Tupo Nawe

Kurudi kwa Gareth Bale England, kufungua milango kwa mshambuliaji nyota wa Man City kutua Hispania

Real Madrid inajiandaa kumtoa mshambuliaji wa Wales,  Gareth Bale,30, kwa pauni milioni 70 kubadilishana na nyota wa Manchester City, Raheem Sterling ,24. (Sky Sports)

Gareth Bale

Chelsea wana mshambuliaji wa Crystal Palace na mchezaji wa timu ya taifa Ivory Coast Wilfred Zaha,26 huku mshambuliaji wa RB Leipzig Tino Werner, 23, akiwa miongoni mwa wachezaji muhimu wanaowawinda ikiwa marufuku dhidi yao itaondolewa. (Express)

Meneja wa Chelsea, Frank Lampard atakuwa na mpaka pauni milioni 150 kwa ajili ya dirisha dogo la usajili mwezi Januari ikiwa klabu hiyo itaruhusiwa kusajili wachezaji tena baada ya kuzuiwa kufanya hivyo.(Telegraph)

Manchester United na Liverpool wamehusishwa na tetesi za kutaka kumsajili Werner lakini klabu hizi za England zimeieleza RB Leipzig kuwa hazina nia ya kumfanya mshambuliaji huyo kuicha klabu yake.(Mirror)Wilfred Zaha

Manchester United imemfanya kiuno wa pembeni wa West Ham Declan Rice,20, kuwa mchezaji wanayemtolea macho kwa kipindi kijacho cha majira ya joto. Lakini huenda akafikishwa kwenye klabu hiyo mapema mwezi Januari (Goal)

Chelsea imeingia katika kinyang’anyiro cha kumnasa mshambuliaji wa Lyon Moussa Dembele,23, huku mchezaji huyo wa zamani wa Celtic macho yake yakiwa Manchester United.(Mail)

Kocha wa zamani wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho angependa kuifundisha Bayern Munich, kwa mujibu wa kiungo Bastian Schweinsteiger.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW