Picha

Kutana na director wa video mpya ya Joh Makini, studio yake imemcost zaidi ya $100,000

Nisher ni msanii, producer wa muziki na director wa video ambaye makazi yake ni jijini Arusha.

Ameanza kujulikana miezi ya hivi karibuni tu lakini uwezo wake na muonekano wake ni wa kimataifa. Kuna vingi vinavyovutia kutoka kwake. Hivi karibuni amedirect video mpya ya Joh Makini – Sijutii.

Joh Makini na Nisher wakiwa location wakati wakishoot video ya Sijutii

Ana upekee mwingi ukianzia na mwonekano wake ambao unaweza kukufanya udhanie ni mmarekani kama ukikutana naye.

Kingine ni kuwa mmiliki wa studio yenye gharama zaidi pengine kuliko studio nyingi sana nchini.

Hivi karibuni Nisher alizungumza na mwandishi wa makala hii ambaye alitaka kumfahamu zaidi kutokana na kuanza kuwika jijini Arusha na sasa nchi nzima ikianza kumtambua na pia kutaka kujua studio yake ya muziki ina gharama gani.

“Vyombo havikununuliwa kwa siku moja, “alisema Nisher. Ni mkusanyiko wa manunuzi toka mwaka 2005 hadi leo maana mwaka huo nilikua Marekani na miaka iliyofuata nikaenda nchi nyinginezo kama Holland, Dubai, Israel, Egypt na South Africa kimasomo, kimatembezi na kitalii.

Nisher alipokuwa nchini Misri

Huko Huko nikaweza kununua vifaa vingi sana tena kwa bei nzuri. Vinginevyo ni baba alinisupport kama kuwekeza katika kipaji/ujuzi/sanaa nilizonazo maana ni nyingi kwa kweli. Sasa ukichanganya na matengenezo ya studio (taa, fabrics, materials n.k mpaka hapo ilipo kwa haraka haraka thamani ya studio ni kama zaidi $100,000$ (zaidi ya shilingi milioni 150).Ila vitu vyote havikupatikana kwa siku moja. Ni mkusanyiko wa manunuzi toka mwaka 2005 mpaka kesho.

Nilipokua nchi za nje nilikua nasoma lakini pia nilikua nikifanya kazi (Graphic Designes na Video & Music Production so hela niliyoipata nilikua naitunza. Pia Mara nyingi my dad Geordavie (Mchungaji/Mhubiri) ameamini sana katika talents zangu na ujuzi nilionao maana yeye ndiye aliyenifundisha kazi hizi mwanzoni. Kwahiyo amekua akinisupport kwa kiwango kikubwa zaidi.

Kuhusu kujigawa kikazi akiwa kama director wa video,mtayarishaji wa muziki, mtunzi, muimbaji n.k

Dah! hapo ni pagumu japo nakuaga na ratiba katika kila ninachofanya (Work Plan). Rafiki yangu/Manager Addy John ( AJ ) amekua akinisaidia sana kuplan utendaji wangu wa kazi, kwamba wakati gani nifanye nini na wakati mwingine nifanye nini kutegemeana na mtiririko wa kazi kwa sababu nina kazi nyingi mno! Singer(Artist)/Song Writer/Composer/Graphics Designer/Music Producer/ Video Director & Editor/ Phototographer/ IT & web desiner nk . Lakini muda mwingi zaidi siku hizi nautumia studio kwaajili ya kujenga jina!
Kusema ukweli silali vya kutosha! Nafanya kazi masaa 18 kila siku, na wakati mwingine nakesha kwa masaa 72 (siku 3) bila kufunga jicho.

Kuhusu kuiweka studio yake Arusha

Nilifungua studio Arusha kwasababu Arusha(ATL – Arusha-Town-Luxury) ndio mji wangu na ni mji wenye vipaji vingi vya kila aina lakini vichwa ( ma-producer ) vyenye International ideas ni vichache. Hilo ndo lililonisukuma kufungua studio Arusha.
Dar watu wengi tayari wana idea ya kufaya International Music ila basi tu hawafanyi kivile. Pia studios nzuri pia zipo Dar, nikaona kwanini tubanane wakati nina jiji langu hapa. Acha kwanza Nirepresent ATL to the fullest!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents