DStv Inogilee!

Kutana na Mtanzania ‘Danzak’ aliyeacha kazi ya urubani Oman na kukimbilia kwenye muziki wa Bongo Fleva (+video)

Kama bado huamini kuwa muziki wa Bongo Fleva umekua basi utakuwa nyuma ya muda kwani Watanzania wanaoishi nje ya nchi hao wameona kuwa kuna fursa ya kuutumia muziki huo kimataifa, kama msanii wa muziki Danzak ambaye yeye ni Mtanzania anayeishi nchini Oman.

Danzak kwenye mahojiano yake na Bongo5, amesema kuwa ameamua kuachana na kazi hiyo kwa sasa ili ajikite kwenye muziki, huku akiahidi baadae kutumikia kazi zote kama mambo yataenda sawa kwenye muziki.

Danzak kwa sasa ameachia video ya wimbo wake mpya wa Fallin’, na tayari ameshafanya kolabo na Tekno. Unaweza ukautazama video hiyo hapa chini

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW