Burudani

Kutana na Producer Emmy Dee Anayesifika Kwa Historia Ya Kuvumbua Vipaji Na Kuwafanya Mastaa Kenya!

Hivi umeshawahi kaa nchini na ukajiuliza kama kuna waatarishi wa muziki ambao wako na wananeema ya kugundua vipaji, kuvikuza kwakuvilea hadi kufikia kiwango cha kuwa mastaa? Pengine kwa harakaharaka hivi unaweza kulichukulia poa swala hili.

Lakini unajua ya kwamba swala hili sio la kawaida na sirahisi? Je unajua sio waatarishi wote Wa muziki wakali wanaweza fanya jambo kama hili, maana wengi hawapendi maadhila wala karaha zinazoletwa na wasanii chipukizi, hivyo hukimbilia kufanya kazi na mastaa wakubwa ambao tayari wamejitengenezea majina, wanamuonekano na sifa tele ukiacha nyuma kuwa wanapesa na mali chungu nzima.

Katika swala hili nchini Kenya, mtayarishi wa muziki maarufu kama Producer Emmy Dee anasifika kwakua kati ya watayarishi wa muziki ambao wamewahi kuvumbua, kukuza, nakufikisha wasanii wachanga kwenye hatau zakua mastaa tajika kwenye majira tofauti.

Mtayarishi huyu Wa muziki kutoka Kenya, alianzia kazi yake ya muziki mwaka Wa 2004 , na amekua akivumbua, kukuza na kuwapandisha wasanii hadi hatua za kuitwa mastaa. Kipindi hicho akianza, kuna mastaa wa awali aliowaweka kwenye ramani kama Double S, Daddy Sele, Prince Adio nawengine wengi. Halafu katika awamamu ya pili, akawakuza na kuwalea wasanii walio sumbua miaka ya 2007-hadi sasa. Wakiwemo Neto, Fidempa, Sudi Boy, Kundi la Rude Boys, Dogo Richie, Majid, na wengine wengi.

Japo wengi walipofanikiwa walilewa ufanisi na kutuliza, wengine wakahamia nchi za nje, na kuna wale ambao wapo kwenye game ya muziki hadi sasa, kama vile Sudi Boy na msanii mkali Dogo Richie.

Kitu ambacho kimemfanya Emmy Dee kuwa gumzo kwasasa kwenye media za nchini Kenya, ni baada ya mwishoni mwa mwaka jana kuwaletea wakenya wasanii wawili wapya ambao tayari kazi zao zimekubaliwa mia kwa mia na mashabiki wa muziki nchini humo.

Akijadiliana na Dj Flash na mtangazaji mwenza Seli kadoti Amtabi wote wa Radio Citizen nchini Kenya, Mzazi Willy M Tuva alifafanua kwa kina jinsi Emmy Dee anastahili kupewa heshima ya kipekee.

Wasanii wapya ambao amewatoa na kazi zao zimekubalika kwa haraka na Mashabiki ni Winta na Adasa. Ambao kwa kasi wanayopaa nayo kwenye kiwanda cha burudani kweli inampa Emmy Dee nafasi yakua na heshima ya kipekee nchini Kenya.

Imeandikwa na Muandishi Changez Ndzai- Kenya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents