Kutana na Twiga warefu zaidi duniani kutoka Tanzania wanaosafisha meno yao kwa kutumia ndege
Katika hali isiyo ya kawaida Twiga wanaopatikana magharibi mwa Mkoa wa Kilimanjaro hapa nchini Tanzania wamekuwa na desturi ya kusafisha meno yao kupitia aina ya ndege wadogo wajulikanao kama oxpeckers.
Twiga hao wamekuwa kivutio kikubwa kwa wageni wanaozuru mbuga hiyo kufuatia kuwa na tabia hiyo ya kuacha kinywa wazi ili ndege hao waweze kusafisha meno hayo kutokana na mabaki ya vyakula pamoja na wadudu wanaopatikana kwenye mdomo huo.
Mpiga picha mmoja raia wa Moscow ajulikanae kwa jina la Julia Sundukova ambaye amepiga picha tukio hilo ameuambia mtandao wa Daily Mail kuwa nimaajabu kuona kitendo hicho kinachofanywa na Twiga hao wanaopatikana mbuga ya Kilimanjaro nchini Tanzania ukilinganisha na wasehemu nyingine duniani.
Licha ya kuwa ndege hao wadogo wajulikanao kama Oxpecker wanapata chakula kupitia kwenye meno ya Twiga hao lakini pia mnyama huyo mrefu kuliko wote hutoa ulimi nje ili kuruhusu shukhuli hiyo kuwa nyepesi zaidi.
Picha hizi zilizopigwa kwenye mbuga ya wanyama ya Kilimanjaro zinaonyesha ni kwa kiasi gani Twiga hawa walivyokuwa na uhusiano mzuri na ndege hawa aina ya oxpecker.
Ndege hawa husafisha meno ya Twiga na kutoa mabaki ya chakula yaliyosalia kwenye mdomo ambayo expecker hutumia kama sehemu ya chakula.
Julia Sundukova kutoka Moscow ndiyo aliyepiga picha hizo na kusema kuwa ameshangazwa na kitendo hicho cha Twiga hao wa Kilimanjaro ukilinganisha na wasehemu nyingine.
Sundukova amenukuliwa akisema kuwa ‘kila Twiga waliyepata bahati ya kukutananae alikuwa na ndege waliyozunguka mdomoni.
Wanasafisha meno kwakutumia ndege au wanawala kabisa??
nawaona hao ndege tunawaita buffaro weaver
Admin kwa uelewa wake kutafuna ni kusafisha meno. Labla kama baada ya hapo wanawatema.
Daa nchi hii inakilakitu.
Bongo lala
Proudly Tanzania
Hapana. Ndege hao wanakula vyakula vilivyo baki karika meno ya twiga
Fille Kabungurura muhhh
Hao ni waharibifu
Hiyo ndo kitaalamu inaitwa Symbiosis
Uwongo bhana
Ahsante kwa kutuonesha utalii wa ndani.
daaa kumbeee,,,,ndiomana saivi kila nikiwinda ndege siwaoni babeki kumbe kuna vitwiga vinakula kitoweo changu