Habari

Kutana na vijana wa Tanzania wanaotengeneza app itakayotumika kununulia tiketi za movie ama mechi za mpira kwa kutumia smartphones

Josephat Joffrey Mandara, Godluck Akyoo, Mwasapi Kihongosi na Alan Abbas ni vijana wadogo waliomaliza elimu ya sayansi ya komputa kwenye chuo kikuu cha Dar es Salaam na mmoja masomo ya biashara. Baada ya kumaliza masomo yao, hawakutaka kabisa kuajiriwa na kila mmoja kuwa na nia ya kuanzia kampuni.

2013-06-21 18.30.09
Kutoka Kushoto: Josephat Joffrey Mandara na Godluck Akyoo, Ticketing Made Easy (TiME)

Josephat na Mwasapi wamefanikuwa kuwa na kampuni yao iitwayo Dephics huku Godluck akiwa nayo ya kwake iitwayo Cityweb Technologies.

Kwa pamoja wameungana kuja na ugunduzi wa application ya computer ambayo ikikamilika na kuingia mtaani itabadilisha kwa kiasi kikubwa mfumo wa ukataji tiketi katika majumba ya sinema ama kwenye show za muziki nchini. Application hiyo inaitwa Ticketing Made Easy (TiME).

“Wazo lilikuja kwamba kwanini watu wanasumbuka sana katika masuala ya kununua tiketi, tukasema kwa kuanzia kabisa tutaanza na uuzaji wa tiketi katika sehemu za movie na baadaye sehemu zingine kama ni party, concert, mpira,” anasema Josephat.

Ameongeza kuwa walengwa wa kubwa wa mfumo wao ni wamiliki wa smartphones kwakuwa kadri muda unavyozidi kwenda watumiaji wa simu hizo wanaongezeka.

“Ile tiketi utatumiwa kama picha kwenye ile application na utakuwa nayo, kuna sehemu ambayo hizo tiketi zitakuwa zinahifadhiwa, ukishaiagiza hiyo tiketi kabla hujailipia kuna sehemu ambayo zitakuwa zinakaa kwamba ni pending tickets au unpaid tickets, ukishailipia tu inaingia kwenye your tickets. Kwahiyo siku unapoenda kwenye shughuli kama ni movie kama ni mpirani tutakuwa na vifaa vyetu ambavyo ni scanner za kuhakikisha ile tiketi. Kwahiyo wewe utakuwa na simu yako tu scanner itakuwa inamulika baada ya hapo unaruhusiwa kuingia ndani,” anaeleza.

“Kwahiyo tunapunguza ule mzunguko ambao watu wanao mtu kutoka kwenda kutafuta tiketi sehemu nyingine lakini tunachukua pia jukumu la kusaidia watu wanaoandaa shughuli mbalimbali kupunguza gharama sababu unapoprint zike tiketi utatumia gharama, kuna watu itabidi uwalipe kukuuzia zile tiketi.”

Hata hivyo amesema mfumo huo bado upo kwenye hatua za wazo linaloendelea kuboreshwa zaidi japo mchoro mzima na jinsi itakavyofanya kazi upo tayari.

Kwa sasa vijana hao wameingia kwenye fainali ya shindano la ubunifu wa masuala ya IT litakalofanyika wiki ijayo nchini Uganda.

“Tulipata kusikia tangazo kwamba kuna competition ambayo inahusisha vijana ambao wameanzisha biashara ndio zipo kwenye hatua za mwanzo au zinaendelea lakini wanahitaji msaada ili wafike katika malengo waliyojiwekea na kile wamekuwa wanakiona. Baada ya kupata hiyo taarifa tulichukua hatua ya kushiriki. Kwahiyo sasa tupo kwenye fainali lakini hiyo inahusisha nchi za Afrika Mashariki.”

Sikiliza interview nzima hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents