Habari

Kuteua Jaji Mkuu ni kazi ngumu – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli ameeeleza kuwa kuteua Jaji Mkuu ni kazi ngumu huku akisema ni lazima ujue historia na tabia zake ikiwa ni pamoja kuangalia kama ataweza kuendana na dhamira ya kupambana na rushwa.

Rais Magufuli ameyazungumza hayo leo , wakati wa kumuapisha Jaji Mkuu, Profesa Juma baada ya kumteua jana Jumapili. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam

“Nilifanya hivyo si kwasababu kwamba majaji walikuwa hawafai, majaji wote ni wazuri sana na mnafanya kazi yenu nzuri sana lakini moja lililo kubwa sikutaka kuteua jaji baada ya mwaka mmoja nateua tena Jaji au baada ya miaka miwili anastaafu, nilitaka nikiteua akae miaka hata 10 awe anatujaji tu wote tutakaokuwepo. Kwahiyo niliyazingatia hayo lakini na mengine mengi including historia lakini nakuangalia zaidi kwamba je huyu nitakaye mteua dhamira yangu inaridhika nae kupambana na rushwa? Kwasababu rushwa ni janga kubwa ,” amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alisema kumteua Jaji Mkuu ni kazi ngumu, lazima ujue historia na tabia zake, pia kuangalia iwapo ataweza kuendana na dhamira yake ya kupambana na rushwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents