Burudani

Kutoka kwa Damian Soul, namna mbili za msanii kutoa wimbo

Msanii wa Bongo Fleva, Damina Soul ameeleza namna mbili za msanii kutoa nyimbo.

Akizungumza na Daladala Beat ya Magic FM, muimbaji huyo amesema namna ya kwanza ni pale msanii anapotoa wimbo kwa mashabiki wake kutokana na mapenzi alionayo kwao, na pili ni kutoa wimbo  kwa ajili ya biashara.

“Hapa kuna angle mbili, angle za kibiashara na angle za kimapenzi na sasa inatengement unataka kufanya nini. Wakati mwingine sio mbaya kufuata audience inavyotaka kwa sababu wewe kama mwanamuziki unaweza ukacheza pande zote mbili ili uweze kuimarisha kile unachotaka kwao,” amesema na kuongeza.

“Na nikiangalia hata nimejifunza kwa ma-legend kama Bob Marley walifanya miziki yao wanayoipenda lakini walifanya miziki mingine kwa kuwaangalia watu wao wanataka nini,” amemaliza kwa kusema.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents