Soka saa 24!

Kutoka mchezaji hadi kuwa na ndoto za U-bilionea, huyu ndiyo David Beckham na Inter Miami MLS yake

Bila shaka kwenye ramani ya mchezo wa soka jina la David Bekham si geni maskioni mwa watu, kwani ameichezea timu yake ya taifa ya Uingereza kwa mafanikio makubwa huku wengi walivutiwa zaidi na kipaji chake alipokuwa kwenye klabu ya Mashetani wekundu Manchester United.

Tuachane na hilo la umahiri wake wa namna alivyoweza kuunyanyasa mpira katika zama zake. Ni zaidi ya miaka nane sasa imekatika toka David Beckham kuwa na ndoto za kuwa miongoni mwa watu wanaoitwa mabilionea huku akiamini kuwa kupitia soka kama mchezo aliyokulia na kuupenda zaidi kwenye maisha yake hasa pale kwenye mitaa ya jiji la London atafanikisha hadhima yake hiyo.

David Beckham's long awaited MLS franchise is finally close to joining the American league

Hamu kubwa aliyonayo kwa sasa baba huyu wa watoto wanne ambao ni
Brooklyn Beckham, Romeo James Beckham, Harper Seven Beckham na Cruz Beckham na kutaka kushuhudia klabu yake ya Inter Miami inapata kushiriki ligi kuu nchini Marekani (MLS ) na yeye kupata kucheza walau michezo kadhaa kama mmiliki.

Habari njema kwake ni pale anapofahamu kuwa klabu ya Inter Miami itaingia rasmi kwenye ligi kuu ya Marekani (MLS ) ifikapo msimu wa mwaka 2020 wakati yeye akiwa kama kioo wa timu hiyo mbele ya jamii.

Hata hivyo jina la Inter Miami halikupatikana kirahisi bali lilipita kwenye michakato kadha mpaka kupatikana jina kamili ambalo ni Club Internacional de Futbol Miami kwakifupi ( Inter Miami ).

Umiliki wa klabu hii mpya yenye uwanja wake wa kisasa kabisa, kama inavyofahamika kuwa miradi mikubwa ya kimaendeleo au kampuni maranyingi humilikiwa na mtu zaidi ya mmoja kwa jina la kigeni hutwa ‘shareholder’ ambao huweka fedha zao kwa pamoja ili kufikia adhima ya jambo fulani.

Mwaka 2007, alipoamua kujiunga na klabu ya Marekani ya LA Galaxy moja ya makubaliano ambayo yakifanyika kwenye usajili wake ilikuwa ni kuwa sehemu ya umiliki wa timu hiyo ya MLS huku akipata punguzo fidhi la dola za Kimarekani milioni 25 hii ilikuwa ni mara baada atakapomaliza kuitumikia kama mchezaji.

Ndipo mwaka 2013 akaanza mipango ya kuwa na klabu yake ambapo hapo awali ilikuwa ikijulikana kama ‘Miami Beckham United ambapo baadaye ndipo jina la Inter Miami likapatikana na kuanza rasmi kutumika Januari 28, mwaka 2018.

Beckham ni mmoja kati ya wamiliki wa Inter Miami, wawekezaji wengine ni Simon Fuller ambaye ni kocha wazamani wa Spice Girls (akishirikiana na mke wa Beckham, Victoria), Bilionea kutoka nchini Bolivia ambayo inapatikana Amerika ya Kusini, Marcelo Claure, Mfanyabiashara wa Florida, Jorge akiwa na Jose Mas, pamoja na Mkurugenzi wa benki ya Japani, Masayoshi Son.

Badge, hii ilikuwa ni sehemu muhimu kwa klabu hiyo ambapo rangi zake ‘Nyeusi na Pinki zilianza kuwa rasmi Septemba mwaka 2018.

Inter Miami was the chosen name, with the crest and team colours a notable black and pink

Yenyewe husanifu hasa jiji la Miamia ikiwa na ndege wawili waliyoegemeana. Kuelekea kwa juu kunazungukwa na jina la timu hiyo huku kwa chini kukiwa na maandishi ya kiroma ‘MMXX’ yakiwa na maana mwaka 2020, ikiwa huu ndiyo mwaka utakaoingia rasmi MLS.

Mipango ya uwanja, wakati ulipoanzishwa Inter Miami maswali mengi watu waliyokuwa wakijiuliza ni juu ya kuwa na dimba lake la nyumbani.

Beckham na wamiliki wengine ndipo wakaadhimia kujenga uwanja utakaoweza kubeba wafanyakazi 25,000 katika Miami Freedom Park lakini hata hivyo ni dhahiri kuwa mipango hiyo haitakamilika kunako mwaka 2020. 

The Lockhart Stadium - which will be Miami's temporary home in 2020 - is horribly rundown

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW