Kuwasaidia watu wengine ni njia ya kumshukuru Mungu-Mengi

Bw MengiMwenyekiti Mtendaji wa IPP, Bw. Reginald Mengi amesema ushirikiano katika kuisaidia jamii hususani watu maskini wasio na uwezo, ni jambo la heshima kwa binadamu na njia bora ya kuuthamini utu wa mwanadamu

Bw Mengi


 


Na Bilham Kimati



 


Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Bw. Reginald Mengi amesema ushirikiano katika kuisaidia jamii hususani watu maskini wasio na uwezo, ni jambo la heshima kwa binadamu na njia bora ya kuuthamini utu wa mwanadamu.

Bw. Mengi alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwahutubia wanachama wa Lions Club ya Dar es Salaam Pwani katika siku ya kimataifa ya Lions kuwapokea na kuwatambulisha wanachama wapya.

Katika hafla hiyo, wanachama sita walijiunga na Lions Club ya Dar es Salaam Pwani baada ya kula kiapo cha utii.

Bw. Mengi ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema siku ya Kimataifa ya Lions, ina umuhimu mkubwa kutokana na ukweli kwamba wanachama wapya wenye moyo wa kujitoa kuwatumikia watu wengine wanatangaza utayari wao wa kuisaidia jamii.

Alisema Lions Club ya Dar es Salaam Pwani chini ya uongozi wa Rais Shakil Ansari, inastahili sifa kutokana na mchango wake mkubwa katika jamii katika nyanja mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wahanga wa moto, mafuriko, wahitaji wa huduma ya afya na kuwatembelea watoto waliopo gerezani upanga jijini Dar es Salaam kuwafariji na kuwatia moyo kuwa raia wema.

“Kuwasaidia watu wengine ndiyo njia nzuri ya kumshukuru Mungu kwa kipato mtu alicho nacho. Tupo jinsi tulivyo kwa rehema za Mwenyenzi Mungu.

Ukarimu kwa wengine uwe ni utamaduni unaofaa kuendelezwa kama wafanyavyo wanachama wa Lions Club ya Dar es Salaam Pwani,“ alishauri Bw. Mengi.

Naye Makamu Gavana wa Wilaya Lions Club Dar es Salaam Pwani, Bw. Abdul Majid Khan alisema Lions Club iliyoanzishwa mwaka 1917 na mfanyabiashara mmoja huko Marekani, ina wanachama milion 1.3 duniani kote.

“Tukiwa wanachama wa Lions, hatuna budi kutumia nguvu, uwezo na raslimali zetu kuwasaidia wenzetu wahitaji ikiwa ni sehemu ya kuuheshimu utu wa mwanadamu,“ Alisema Bw. Khan.


 


Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents