Michezo

Kwa ofa hii ya tatu kutoka Barcelona Chelsea wanaweza kumwachia Willian?

Kwa ofa hii ya tatu kutoka Barcelona Chelsea wanaweza kumwachia Willian?

Klabu ya Barcelona ya Catalunya nchi Uhispania umetuma ofa nyingine kwa mara ya tatu katika klabu ya Chelsea kuisaka saini ya winga wa timu hiyo Mbrazil Willian.

Willian amekuwa akiwindwa na vilabu vingi sana barani Ulaya hasa Barcelona,pamoja na Manchester United vikionyesha kuridhishwa na kiwango cha winga huyo,ingawa Barcelona wameonesha nia kubwa ya kumtaka winga huyo Mbrazil.

Chelsea walizitupilia mbali ofa za mara ya kwanza ambazo zilikuwa ni Euro mil 53 lakini ofa ya mara hii inakadiriwa kufikia Euro mil 55 kiasi ambacho kimeleta maswali mengi kwa wadau kujiuliza kama Chelsea wanaweza kuipotezea ofa ya mara hii tena,Ingawa kocha mpya wa timu hiyo Maurizo Sarri alionesha kuzungumza na wachezaji wanaotaka kuondoka Chelsea na kusema watayaweka sawa.

Willian ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa msimu uliopita katika klabu hiyo tayari ameifungia Chelsea magoli 44 likiwemo lile aliloifunga Barcelona katika michuano ya UEFA hatua ya 16 bora katika michezo 236 tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2013 akitokea Anzhi ya nchini Urusi.

Chelsea tayari wamefanya usajili wa watu watatu tu ambao ni kocha mkuu wa timu hiyo Maurizio Sarri akitokea Napoli ya Italia pia kocha msaidizi Gianfranco Zola akitokea Birmingham City vile vile kiungo Joginho aliyebadili upepo kwa kuikacha Manchester City na kudai anapenda kuishi London hivyo kuelekea Chelsea aliko kocha wake aliyemfundisha akiwa Napoli Sarri. .

 

By Ally Jei

Related Articles

One Comment

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents