Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Burudani

Kwa Orezi, Vanessa Mdee ni zaidi ya Davido

By  | 

Vanessa Mdee ni miongoni mwa wasanii wachache wa Bongo Flava ambao wamekuwa wakipambana kuhakikisha muziki wao unafika mbali katika ngazi za kimataifa na hilo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Tumemshuhudia muimbaji huyo akifanya kolabo na wasanii wa nje kama K.O, Orezi, Ice Prince, Reekado Banks na wengine na kote alipopewa nafasi hiyo ameweza kuitumia vizuri. Kwa siku za hivi karibu idadi ya views inaopata wimbo fulani katika mtandao wa YouTube imekuwa ikitumika kama moja ya kigezo kikubwa cha kutambua wimbo umefanya vizuri.

Sasa sikia hii, msanii kutoka Nigeria Orezi mwaka huu ametoa wimbo uitwao ‘Just Like That’ aliomshirikisha Vanessa, ngoma hiyo imefanya kufanya vizuri zaidi YouTube kuliko kolabo aliyowahi kufanya na Davido miaka miwili iliyopita ya wimbo wa ‘Shuperu Remix’.

Ngoma hiyo aliyofanya na Davido ilitoka Mei 1, 2015 na hadi sasa imetazamwa mara 825,084, wakati ile ya ‘Just Like That’ aliyofanya na Vanessa Mdee ambayo video yake imetoka Machi 17 mwaka huu imetazamwa mara 1,121,501. Kwa kutazama kwa angle hiyo Vanessa amekuwa bora zaidi ya Davido.

Pia katika channel ya YouTube ya Orezi ‘Orezi Worldwide’ ambayo ina video 43, kolabo ya Vanessa Mdee ndio pekee iliyoangaliwa zaidi ya mara milioni moja.

By Peter Akaro

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW