Michezo

Kwakuifikisha England nusu fainali kombe la Dunia, meneja Gareth Southgate kupewa mkataba mnono na FA

Meneja wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate ameridhia kuongeza mkataba wake utakao endelea kumuweka hapo hadi mwaka 2022 na kukutana na michuano ijayo ya kombe la dunia.

Southgate mwenye umri wa miaka 48, anatarajia kusaini karatasi za mkataba kabla vijana wapya hawajajiunga na kikosi cha taifa huko St George Park siku ya Jumapili jioni.

Dili hilo linajumuisha kuongezewa kima cha mshahara kwa asilimia 50 hii inatokana na kuiwezesha Uingereza kufika hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia mwaka 2018.

Mkurugenzi wa chama cha soka England (FA), Martin Glenn amesema kuwa hawakuweza kukamilisha hiyo biashara na uongozi wa Southgate nchini Urusi na lengo kuu ni kuwa kwenye nafasi ya nne duniani kwenye viwango vya FIFA.

Southgate anatarajiwa kuwa na mkutano na waandishi wa habari Alhamisi hii huko  St George’s Park ili kutangaza kikosi kitakacho jiandaa na Nations League mechi dhidi ya Croatia na Hispania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents