Burudani

Kwanini ‘Nobody But Me’ ya Vanessa ni video na wimbo bora wa hip hop/rnb Afrika tangu mwaka 2015 uanze!

Wanasema real recognize real. Ili uweze kujua uzuri wa kitu ni lazima uwe na mifano mingi ya kulinganisha kabla ya kuamua kufikia hitimisho.

Wimbo na video ya mpya ya Vanessa Mdee ‘Nobody But Me’ ni kitu ambacho kitakuwa ni kosa kama sisi tunaochambua muziki tukinyamaza na kutoisema dhahabu iliyomo kwenye wimbo huo.

Nilikuwa kwenye redio kwa zaidi ya miaka 10 kabla ya kuingia kwenye uandishi wa masuala ya burudani huu ukiwa ni mwaka wa tatu sasa. Hiyo inamaanisha kuwa kwa zaidi ya miaka 13, sikio langu limekuwa likisikiliza nyimbo nyingi sana za kila kona ya dunia.

Kwa miaka hiyo yote nimekuwa nikisikiliza nyimbo si kama msikilizaji wa kawaida, bali kama jaji kama wale wanaoshirikishwa kwenye mashindano ya muziki duniani.

Wakati mwingi sana pamoja na kuzijaji nyimbo mpya zinazotoka, nimekuwa nikiyatunza tu maoni yangu moyoni au labda kuyashirikisha kwa wenzangu wa Bongo5.

Lakini mara nyingi nimekuwa na desturi ya kuchukua muda na kuandika kitu pale ninapoona kazi nzuri ya kutolewa mfano. Nobody But Me imenipa mzuka huu wa kutonyamaza bali kuusema uzuri wake.

Well, unajua sasa hivi muziki wa Tanzania umebadilika mno. Si ule kama wa zamani ambapo nyimbo kama Mabinti, Cheza Kwa Step, Ghetto Langu, CNN na zingine tulizokuwa tukiziskia kwenye vipindi vya mchana vya redio zetu pendwa.

Nyimbo nyingi sasa hivi ni zile zinazokulazimu ukimbie nazo na wakati mwingine zinakuwa ni kama chotara wa Bongo Flava na muziki wa Nigeria. Ndio maana nyimbo zenye ladha ya ‘Nobody But Me’ ni chache mno kuzisikia.

Kwahiyo kwa Vanessa kufanya wimbo wa R&B, mahadhi ambayo ni kama ‘endangered species’ kwenye redio, hatuwezi kukaa kimya bila kumpa pongezi zake ili muda, nguvu, ubunifu na gharama alizotumia kutengeneza ‘this masterpiece’ zisionakane kama ni bure tu.

Nobody But Me ni ngoma kali. Ni kabila moja na collabo zenye mchanganyiko wa R&B na Hip Hop kama zile ambazo Beyonce amekuwa akizifanya na mume wake Jay Z. Narudia tena kwamba real recognize real’ kwa maana kwamba kama wewe ni mtu unayesikiliza muziki juu juu tu unaweza usielewe hiki ninachokisema.

Vanessa ni genius! Kumwimbisha Kiswahili mtu anayetajwa kuwa rapper namba moja ama namba mbili Afrika Kusini si kitu cha kubeza! Nobody But Me ni wimbo ulioandikwa na kutayarishwa vizuri unaochezeka na kusikilizika vizuri ukilinganisha na nyimbo nyingi za sasa ambazo nyingi zimekuwa ni za kuchezeka zaidi kuliko kusikilizika.

Kwa haraka haraka title ya wimbo inaweza kukufanya udhani kuwa Vanessa angeimba Kiingereza peke yake, lakini kwa kutambua kuwa muziki ni lugha ya dunia, ameamua kukipaisha Kiswahili, lugha yetu ya taifa.

Unaweza kusikia jinsi ambavyo Vee Money ameendelea kupevuka kiuimbaji siku hadi siku na nidhamu yake kwenye kazi hiyo haielezeki.

Video ya Nobody But Me ni kitu kingine kinachoufanya wimbo huu uwe tofauti na zingine na uwe si wimbo tu mkali kwa Tanzania, bali ni wimbo mkali kwa Afrika. Ni video ya kujiachia yenye mandhari tofauti na isiyochosha kuitazama. Ni aina ya video tulizozoea kuziona zikifanywa na wasanii wakubwa wa Marekani.

Kuna haja ya kuzungumzia uchaguzi bora wa nguo zao kwenye video hiyo?

Hakuna shaka kwa video hiyo, Vanessa Mdee ni msanii bora wa kike Afrika Mashariki kwa sasa. Vanessa anawafundisha wasanii wengine wa Afrika Mashariki kuthubutu kwa kufanya nyimbo tamu za Kiswahili zenye sura ya kimataifa.

Vanessa anaipeperusha bendera ya Tanzania kwa nguvu zake zote. Ni muhimu kutambua jitihada zake hizo na kukipongeza kipaji chake.

Kwakuwa ni nyimbo chache kali zenye mahadhi ya R&B na Hip Hop kwa pamoja tangu mwaka 2015 uanze, Nobody But Me haina mpinzani na kwakuwa ni wimbo ulioikutanisha Tanzania na Afrika Kusini, unaufanya kuwa wimbo mkubwa zaidi katika robo hii ya kwanza ya mwaka.

Swali la kama wimbo huo kamuimbia Jux (kitu ambacho kina uwezekano mkubwa) nalihifadhi kwaajili ya siku nyingine!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents