Habari

Kwanini serikali isiwalipe mishahara Madiwani kama inavyowalipa Wabunge?- Mbunge Hamida ahoji (+video)

Mbunge wa Viti Maalum, Hamida Abdallah ameiomba serikali kuwalipa mshahara Madiwani kama inavyotoa kwa Wabunge kwa kuwa wanafanya kazi sawa.

Hamida ametoa kauli hiyo leo, Juni 26, 2018 Bungeni jijini Dodoma wakati akiuliza swali la nyongeza alihoji hivi “Madiwani wanafanya kazi sawa na Wabunge, Kwanini serikali isiwalipe mishahara kama ambavyo Wabunge wanapewa mishahara?

Akitoa majibu ya serikali Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Joseph Kakunda amesema hivi “Ni kweli kwamba Madiwani wamekuwa na mtazamo huo wakuomba kuwe na malipo hayo ya mshahara serikali iliyapokea hata Rais alipohudhuria kikao cha ALAT mwaka jana nilipokea maombi yao na mimi nasema majibu yaliyotolewa pale ndio sahihi hadi hapo serikali itakapotoa maelekezo mengine lakini kwasasa hivi tutaendelea na utaratibu ambao tunaomba mpaka sasa hivi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents