Burudani

Kwanini sio sawa kwa Linex kumlaumu Adam Juma kwa ubovu wa video ya Salima

Ishakuwa wazi Bongo Flava ya siku hizi inahitaji video nzuri ili isonge mbele. Zinahitajika video zenye viwango vya kidunia ili zipate nafasi ya kuchezwa na kuingia kwenye “rotation” ya TV station kubwa Afrika na duniani kwa ujumla.

11023139_1079461352069718_810752740_n

Pengine bila Chibu Dangote kuwekeza hela nzuri kwenye wimbo wake wa Number 1 na kusafiri mpaka kwenye beach za Camps Bay kule Cape Town, South Africa kwenda kufanya video ile, asingekuwa hapa alipo na pengine asingepata hata nguvu ya kwenda tena Nigeria kufanya remix yake na Davido kwa director mkubwa Afrika, Clarence Peters.

Iko wazi video zile za gharama kubwa zenye viwango vya kidunia ndio zimemfikisha pale alipo.

Adam Juma ni legendary wa industry ya video kwenye Bongo Flava. Alikuwepo toka kwenye hatua za kwanza kabisa za hii kitu na haiwezi kukuacha na mshangao ukijua kuwa ‘jamaa’ ndio video director ambaye jina lake limetokea kwenye video nyingi kuliko mwingine yoyote.
Salima ni wimbo mzuri ambao ulihitaji video nzuri zaidi ya video ambayo tunaiona leo hii.

Mwanzo hatukujua nani ni tatizo tukawa hatujui nani anastahili kubeba lawama kwa ubovu wa video ile.Ila Linex amekuwa wazi kwa kudondosha lawama nyingi kwa Adam Juma kuwa amemuangusha mno kwa kuifanya video yake kuwa ya kawaida.

Adam naye hakuwa mpole kwa kuweka wazi kuwa Sunday Mjeda hakuwa amewekeza hela za kutosha ndio maana video ikawa ya kawaida.

Kauli ya Adam inakufanya ushtuke inakuaje kwa msanii A-List kama Linex kuwa “Mbahili” kama kweli anataka kupiga hatua kwenda mbele na sio kurudi nyuma? Tunasikia kila leo wenzake wanavyopishana viwanja vya ndege kwenda kwa Godfather,Clarence Peters,Moe Mussa,Kelvin Bosco na wengine wengi kule Kenya kutafuta ubora wa video zao kwanini isiwe kwake yeye?

Sidhani kama Adam Juma ni tatizo la kukwama kwa video hii kila siku naiangalia video ya Rich Mavoko “Pacha wangu” ni moja kati ya video bora kutoka kwa Adam Juma na Rich Mavoko aliweka wazi kuwa aliwekeza zaidi ya shilingi milioni 10 za Tanzania kupata video yenye ubora ule.

Utapata wapi video yenye ubora ya kuchezwa MTV, Trace, Channel O au Sound City kwa kuwekeza million 3 za kitanzania?!

Ni nani aliruhusu video iende hewani kama ikiwa haina ubora unaotakiwa!?

Iko wazi video director akishamaliza kazi yake anampa msanii video yake na kama ikiwa ina mapungufu msanii anairudisha tena kwa director ili irekebishwe au kufutwa kabisa na kuanza upya kushoot! Je Linex na team yake hawakuona mapungufu ya ile video mpaka video ikiwa ishatoka?!

Ni kweli Adam Juma ana mapungufu yake kama binadamu wa kawaida ila kwa hili la Linex hapana hastahili lawama hizi kumlaumu ni kumuonea. Ikiwa kukodi camera nzuri kama zile za Godfather kwa siku moja ni shilingi milioni 1.5 hadi 2 nje ya hela utakayomlipa kwa ku-direct video yako, utawezaje kupata video nzuri kwa milioni 3 nje ya kukodi camera ya kisasa?!

Video ya Christian Bella ni mfano mzuri mno kwa alichosema Adam Juma. Wekeza hela upate kitu cha uhakika

Imeandika na Heri Best: Instagram: Heri Best, Twitter: Mimi_Heri

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents