Habari

Kwanini watu wa Kigoma kila mara wanaambiwa sio raia wa nchi hii? – Mbunge ahoji

Mbunge wa Kasulu Mjini(CCM), Daniel Nsanzugwanko amesema kuwa watu wa Kigoma wamekuwa wakibaguliwa waziwazi na Idara ya Uhamiaji kwa kuambiwa wao si raia wa Tanzania.

Mbunge huyo amehoji akiwa bungeni mjini Dodoma akitaka kuelezwa kwasababu suala hilo limekithiri katika mkoa huo, Mbunge alianza hivi;

“Swali langu la kwanza ni kuhusu uraia, mwenyekiti nchi hii wananchi walio wengi wanaishi kwenye mipaka ya Taifa hili na katika mipaka ya Taifa hili upo mkoa unaitwa mkoa wa Kigoma sisi tumekuwa wahanga wakubwa Mwenyekiti wa ubaguzi wa waziwazi kabisa tumekuwa ni wahanga wa madhira ambayo hayamidhiliki kupitia wenzetu wa idara ya Uhamiaji nilikuwa naomba sana Waziri Mkuu uje utueleze hawa wananchi wa Kigoma ambao wanasumbuliwa kwasababu au maumbile yao ,sura zao au lugha yao kwanini kila mara wanaambiwa wao si raia na tunajua Mwenyekiti iko mikoa mingi lakini jambo hili kwa mkoa wa Kigoma limekithiri,” amesema Nsanzugwanko.

“Kwa mfano leo limetokea tukio la ajabu kabisa kuna mwananchi amekamatwa anaambiwa aende na wazazi wote wawili uhamiaji wakati sisi tunajua ni mzaliwa wa palepale haya ni madhira makubwa sana inawezekana wenzetu wa uhamiaji wamekosa tu weledi wa kutenda kazi yao itakuwa jambo la msingi sana hili jambo linatukera sana ningeomba lipewe majibu ya moja kwa moja.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents