Habari

Kwenda Marekani sasa utatumia akaunti yako ya mitandao ya kijamii kuomba Visa, Pigo kwa wakosoaji wa serikali na wabaguzi wa rangi

Utaratibu mpya uliopendekezwa mwaka 2018 wa kila mtu anayeomba Visa ya kuingia Marekani wa kutumia akaunti ya mitandao ya kijamii, unatarajiwa kuathiri takribani watu milioni 15 ikiwemo watu wanaoomba kuingia nchini humo wenye matumaini ya kusoma, kufanya biashara, kazi au kuja tu kutembea.

Kwasasa kila mtu anayeomba Visa ya kuingia Marekani atatakiwa kutoa akaunti zao za mitandao ya kijamii, Pamoja na taarifa zingine binafsi kama sehemu ya utaratibu mkali wa utawala wa Trump wa kuhakiki wahamiaji na wageni wote wanajulikana historia zao.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeeleza kuwa, Imefanya mabadiliko hayo kwenye fomu za kuomba visa kwa wahamiaji na wasio wahamiaji zikimtaka muombaji kutoa taarifa za miaka mitano iliyopita za shughuli zao kwenye mtandao wa kijamii, nambari ya simu, barua pepe, safari za kimataifa na ikiwa amefukuzwa kutoka nchi husika.

Pia wataulizwa iwapo mwanafamilia yeyote ameshawahi kuhusika katika matukio ya kigaidi au kujihusisha kwa namna yoyote ile na mambo hayo.

Kwa mujibu wa mtandao wa VOA, Umeeleza kuwa taarifa binafsi juu ya kazi ya muhusika zilikuwa zikitakiwa kwa waombaji wa Visa ambao wanaweka kitisho cha usalama wa taifa hilo. Imekadiriwa waombaji takribani 65,000 kwa mwaka wanashindwa kwenye kipengele hicho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents