AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Kwikset Kevo: App ya simu inayokuwezesha kufungua mlango kutumia simu ya mkononi

We ni mvivu wa kubeba funguo za nyumba? Kama ndio, huenda utahitaji kuwa na Kwikset Kevo kwenye simu yako. Hii ni app itakayokuwezesha kufungua mlango wako bila hata kutumia funguo tena.

article-2384817-1B2756FE000005DC-686_306x323

App hiyo imewezeswa kutunza funguo za kietroniki ambazo utazitumia kwenye smartphone au tablet.

Inavyofanya kazi

Mtumiaji anapowasili kwenye ofisi ama nyumbani, simu hiyo huufungua mlango ‘wirelessly’ kwa kutumia Bluetooth na anaweza kuufungua bila hata kuitoa simu mfukoni. App hiyo kwa sasa ipo kwenye simu za iOS (iPhone) pekee lakini zitaanza kupatikana pia kwa simu Android na BlackBerry.

article-2384817-1B2756EE000005DC-600_306x323

Kubadilisha mlango uweze kutumia funguo za Kwikset-mtumiaji atatakiwa kununua na kuweka kufuli,komeo maalum linaloona na app hiyo.

article-2384817-1B27573C000005DC-78_306x349

Kwikset Kevo inauzwa kwa paundi 144 ikiwa pamoja na kufuli zake.

Ikiwekwa, mtumiaji anaweza kutumia eKeys kwa ndugu na jamaa zake ili kuwawezesha nao kuingia ndani kwa kutumia app hiyo.

Makufuli hayo yanauzwa yakiwa na funguo zake za kawaida ili kumwezesha mtumiaji kuingia ndani iwapo simu yake ikiishiwa chaji ama asipokuwa nayo.

By Daily Mail

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW