MichezoUncategorized

Kylian Mbappé kuvaa viatu vya Pele baada ya kuonyesha makeke yake World Cup?

Kylian Mbappe ni kijana mwenye umri wa miaka 19 ambaye ameweza kuibeba Ufaransa mpaka kushinda kombe la dunia ambapo aliweza kufunga magoli 4.

Mbappe aliweza kuisaidia timu yake hiyo kwa kiwango kikubwa na amefanikiwa kuifikia rekodi ambayo iliwekwa na mchezaji wa zamani wa Brazil Pele, ya kufunga magoli mengi akiwa na umri mdogo na kuisaidia timu yake kuchukua ubingwa wa Kombe la Dunia.

Mshambuliaji huyo wa klabu ya PSG ya Ufaransa, ambaye alichukua tuzo ya mchezaji bora mwenye umri mdogo Kombe la Dunia, amekuwa alitajwa na wachambuzi wengi wa soka duniani kwamba anaweza kufanya mambo makubwa zaidi duniani.

Mchezaji huyo ambaye pia anafananishwa na uchezaji kama wa Ronaldo, ameweza kufunga magoli 22 akiwa kwenye klabu yake ya PSG huku rafiki yake Neymar Jr ambaye anacheza naye kwenye klabu hiyo akifunga magoli 19.

Kutokana na mafanikio hayo, Mbappe amekuwa akiwindwa na vilavu vingi vikubwa duniani. Moja kati ya klabu ambazo zinatajwa kuwinda saini yake ni Real Madrid kwaajili ya kumrithi Cristiano Ronaldo aliyetimkia Juventus.

Kwa sasa Mbappe anatabiriwa kuwa mmoja kati ya wachezaji ambao wataacha alama kwenye soka duniani kama alivyo, Pele, Maradona, Ronadlo De Lima, Cristiano Ronaldo, Leonel Messi, Ronaldinho pamoja na wakongwe wengine. Je wewe una maoni gani kwenye hili?.

By Clinton Abraham Sumari.

Related Articles

2 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents