DStv Inogilee!

Kylie Jenner amnunulia Tyga gari lenye thamani ya $300k

Kylie Jenner amemnunulia mpenzi wake Tyga gari la kifahari aina ya Bentley Bentayga lenye thamani ya $300k kwa mujibu wa mtandao wa TMZ.

Bentley

Kylie amechukua hatua hiyo baada ya Tyga kuficha gari lake aina ya Ferrari na kudai kuwa limeibiwa. Hata hivyo zawadi hiyo ya Kylie inaonekana kama amelipiza kutokana na Agosti 8, mwaka huu kwenye sherehe yake ya kuzaliwa Tyga alimpatia mpenzi wake huyo zawadi ya gari aina ya Maybach ikiwa ni mara ya pili ndani ya miaka miwili mfululizo.

Wawili hao walionekana kwenye gari hilo jipya la Tyga Jumatano hii huko Los Angeles wakati wa sherehe ya rafiki wa Kylie, Jordyn. Tyga amekuwa na wakati mgumu ndani ya mwaka huu kutokana na kufikishwa mahakamani mara kadhaa kutokana na kuandamwa na madeni ya kodi kutoka kwa wenye nyumba wake.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW