Burudani

Kylie Jenner kuja show yake ya TV

Baada ya kuonekana sana kwenye kipindi cha Keeping up with the Kardashians, hatimaye Kylie Jenner ameamua kuja na TV show yake itakayofahamika kama “The Life of Kylie”

Kylie aliyekuwa akidate na rapa Tyga, ana jumla ya watu milioni 94 wakiwa wanamfutilia katika mtandao wa Instagram na milioni 20 kwenye Facebook na Twitter. Takwimu zinazosadikika kumsaidia kupromote show yake hiyo mpya.

Kabla ya kuachana, Tyga na Kylie waliwahi kufikiria kuanzisha kipindi cha TV kitakachokua kikizungumzia maisha yao kwa ujumla. Lakini ndoto hizo hazikuzaa matunda kwani Kylie anatarajia kuachia Tv show yake akiwa mwenyewe.

Tv show ya Kylie hiyo itaanza kuruka ifikapo july 6 mwaka huu.

https://youtu.be/rlHD5EzYgKw

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents