Michezo

LA Galaxy yampigia simu Messi, Arteta akiri utovu wa nidhamu umemgharimu kiungo huyu wa Arsenal

Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, 32, amepigiwa simu na klabu ya LA Galaxy kujadili uhamisho wa kuelekea Ligi ya Soka ya Marekani (MLS). (Express)

Messi amekiri kuwa anahisi kuna “mambo ya ajabu” yanaendelea Barcelona huku kukiwa na ripoti kuwa klabu hiyo ilikodi kampuni ya mitandao ya kijamii kukashifu wachezaji wake. (Mundo Deportivo, via Mail)

Hata hivyo, Messi yungali anaiona Barcelona kama nyumbani kwake licha ya tetesi za kutaka kuihama klabu hiyo. (ESPN)Jadon Sancho

Jadon Sancho

Klabu ya Manchester United inaimani kuwa itamnasa mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund na timu ya taifa ya England Jadon Sancho, 19, mwishoni mwa msimu, lakini kwanza itawapasa kufuzu kwa mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, 23, amesema kuwa anajisikia fahari kuhusishwa na klabu ya Liverpool lakini anahisi kuwa huenda hayupo tayari kujiunga na timu hiyo ambayo anasema ni “timu nzuri zaidi duniani.” (Metro)Timo Werner

Timo Werner akifunga mkwaju wa penati dhidi ya Tottenham Jumatano usiku.

Klabu ya Juventus imewaorodhesha mshambuliaji wa Manchester City na Brazil Gabriel Jesus (22) pamoja na mshambuliaji wa Paris St-Germain na Argentina Mauro Icardi (27) kama kipaumbele katika dirisha l usajili la mwishoni mwa msimu. (Tuttosport – in Italian)

Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, amesisitiza kuwa atacheza kwa moyo wote Chelsea licha ya kushindwa kuihama klabu hiyo katika dirisha la usajili la mwezi uliopita. (Mirror)Olivier GiroudOlivier Giroud aihakikishia Chelsea kuwa atajitolea kwa moyo wote.

Klabu ya Arsenal inamnyatia beki wa Bayer Leverkusen Jonathan Tah, 24, ambaye anaweza kuondoka katika klabu yake kwa dau la euro milioni 40 mwishoni mwa msimu. (Bild – in German)

Kiungo wa Leverkusen na timu ya taifa ya Ujerumani Kai Havertz, ambaye anahusishwa na tetesi za kuhamia Liverpool, anaweza kuruhusiwa kuihama klabu yake mwishoni mwa msimu, amedokeza mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo. (Goal)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amekiri kuwa hakumpanga kiungo Matteo Guendouzi, 20, katika mchezo dhidi ya Newcastle kutokana na utovu wa nidhamu walipokuwa katika mapumziko Dubai hivi karibuni. (Mirror)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents