Michezo

La Liga yagoma kumuachia Neymar wanasheria wavamia (Video)

Shirikisho la soka nchini Hispania limeingilia kati usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Brazili, Neymar Dos Santos kujiunga na Paris Saint-Germain kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 198 kiasi ambocho kinamfanya kuweka rekodi ya dunia akitokea Barcelona.

Zikiwa zimesalia saa chache kuhitimisha kwa usajili huo wa Neymar kumeibuka wingu zito katika usajili huo unaotarajiwa kuvunja rekodi ya dunia, chama cha soka cha nchi hiyo kimesema PSG walishajaribu kutuma dau hilo kwa Barcelona ili kujaribu kuvunja mkataba wa mshambuliaji huyo lakini La Liga walikikataa kiasi hicho cha pesa.

Uhamisho wa mshambuliaji wa Barcelona, Neymar umepingwa vikali na La Liga huku ikigomea sheria inayotumika kumsajili mchezaji huyo

Wanasheria wa PSG wamewasili katika shirikisho hilo (La Liga) mjini Madrid  leo  Alhamisi katika kuhakikisha wanazima jaribio la La Liga kumzuia mbrazili huyo mwenye umri wa miaka 25.

Tayari La Liga siku ya leo imetoa taarifa kuwa wamewasiliana na wanasheria wa mchezaji huyo “Tunaweza kuthibitisha kwamba wanasheria wa mchezaji walikuja katika ofisi zetu leo asubuhi ili kukubaliana katika hilo na si tumewakatalia na hiyo ndiyo habari pekee tunayoweza kusema”. Shirikisho hilo La Liga limetoa taarifa hizo.

Neymar atua Porto kwa vipimo vya afya

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents