Tupo Nawe

Laana ya Rais Bouteflika yaendelea kuwatafuna Waalgeria, Wananchi waendeleza maandamano kumpinga kiongozi wa muda

Kwa mara ya kwanza katika muda wa wiki saba polisi wa Algeria wamerusha mabomu ya kutoa machozi leo Jumatano kuwatawanya waandamanaji, hasa wanafunzi katika mji mkuu wa Algeria, Algieria.

Waandamanaji hao walijitokeza kufuatia wito wa muungano wa vyama vya wafanyakazi kupinga kuchaguliwa kwa spika wa baraza dogo la Bunge, Abdelkader Bensalah kuwa rais wa muda.

Vyama vya upinzani nchini humo pia vinapinga kuchaguliwa kwa Bensalah, ambaye alikuwa mshauri wa karibu wa Rais aliyeondoka madarakani, Abdelaziz Bouteflika, kufuatia kishinikizo la wananchi.

Hapo jana Rais wa muda Bensalah alihutubia taifa na kuahidi uchaguzi huru na wa haki katika muda wa siku 90 na kuwataka watu kuacha maandamano.

Wanafunzi hao waliokuwa wanaandamana leo wamekuwa wakipaza sauti zao wakisema “hawajatusikia na tutaendelea kuandamana.” .

Wanafunzi, vyama vya kisiasa, pamoja na vyama vya wafanyakazi wanataka kuwepo na kipindi cha mpito kitakachofanya mageuzi makubwa ya utawala na kupanga uchaguzi ulio huru na haki.

Hata hivyo mkuu wa majeshi ya Algeria, Luteni Jenerali Ahmed Gaed Salah, amesisitiza kwamba ni lazima katiba ya nchi kuheshimikwa wakati wa mabadiliko haya.

Kwa mujibu wa katiba, Rais wa nchi akiachia madaraka kwa sababu yeyote ile, ni spika wa baraza dogo la bunge ndiye anaechukua madaraka kwa siku 90 wakati ambapo anatayarisha uchaguzi wa rais mpya.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW