Habari

Lady Gaga apigwa marufuku kukanyaga Indonesia

Msanii anayesifika kwa utofauti wake kimavazi na kimuziki Lady Gaga amepigwa marufuku na Serikali ya Indonesia kupiga show nchini humo kwa sababu zinazosemekana ni za kimaadili na kidini.

Lady gaga ambaye alishauza ticket zaidi ya elfu hamsini amelazimika kuifuta show hiyo baada ya kunyimwa kuingia nchini humo kwa madai kwamba anavaa kinyume na maadili ya nchi hiyo na yale ya Kiislam na zaidi mfumo wake wa kucheza utaweza kupelekea kuwaharibu wananchi wa Indonesia kwa kuwafunza yasiyokubalika kijamii nchini humo.

Lady Gaga hajatoa tamko lolote kufuatia kufutiwa visa ya kuingia nchini humo ila serikali hiyo imebaki kusisitiza hawawezi kumruhusu kuingia nchini humo,na si yeye tu bali ni msanii yeyote wa kigeni ambaye anaweza kutishia ukiukaji wa maadili nchini humo.

Wananchi wa Indonesia ambao walikua wamenunua tickets za show hiyo wamesikitika na kutaka serikali kutokubaki nyuma na kufungwa pigu za udini na kukandamizwa na wachache na kutoskikiliza matakwa ya wengi.

Wadau mnaionaje?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents