Burudani

Lady Gaga avaa Nyama!

Mwanamuziki mwenye umaarufu mkubwa kuliko wote duniani kwa sasa,Lady Gaga,aliwaacha wengi midomo wazi usiku wa Tuzo Za Video za Muziki, MTV VMA’S zilizofanyika usiku wa Jumapili mjini Los Angeles Marekani,baada ya kuibuka akiwa amevaa nguo ilyotengenezwa na nyama ya ng’ombe.

Kituko hicho kilishuhudiwa na wengi waliokuwa katika ukumbi huo pale ambapo mwanamuziki huyo alitunukiwa tuzo ya Video bora kupitia wimbo wake wa ‘Bad Romance’ na kutokea akiwa amevaa gauni,pochi na viatu vyote vikiwa vimetengenezwa na nyama.

Lady Gaga alisema gauni hilo lililokuwa na uzito wa paund 40 pamoja na viatu ilitengenezwa na designer Franc Fernandez akitumia nyama aina ya ‘Matambre’ kutoka Mexico.

I wonder dada huyu ataibuka na lipi tena baada ya Nyama!

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents