Burudani ya Michezo Live

Lady Jaydee ajibu iwapo ni kweli wasanii wanaogopa kumshirikisha sababu nyimbo zao hazitachezwa Clouds FM (Audio)

Kumekuwepo na imani kuwa wasanii wengi wanaogopa kumshirikisha Lady Jaydee kwasababu wanaamini Clouds FM haitoishia tu kutoucheza wimbo huo bali hata zingine zijazo.

13116585_588064311355663_1248451015_n

Clouds FM na Lady Jaydee wana tofauti ambazo hadi sasa hazijamalizika.

Muimbaji huyo wa Ndindindi amefanikiwa kuelezea suala hilo kupitia kituo cha redio cha Nyemo FM cha mjini Dodoma alikoenda kwaajili ya show yake iliyofana ya Naamka Tena Concert.

“Inawezekana pia lakini hawawezi kusema labda moja kwa moja,” Jide alimjibu mtangazaji wa redio hiyo, Winston Makangale.

“Lakini pia sio vizuri umwongelee mtu ambaye hujui mawazo yake yanafikiria nini au pengine unaweza ukaongea hivyo halafu ikawa sio hivyo ukawa umemsingizia,” aliongeza.

“Kwahiyo nafikiri hilo tuwaachie wao kila mmoja atakuwa anajua kwa nafsi yake kama anaweza au hawezi na sababu zipi zinazopelekea aweze na sababu zipi zinazopelekea asiweze. Lakini la msingi kila mmoja afanye muziki wake kwa nafasi yake na watu waweze kuburudika.”

“Mimi sina tatizo na mtu yeyote ambaye atakuwa yupo tayari kufanya kazi na mimi,” Jaydee alijibu baada ya mtangazaji kusema anatamani kusikia collabo yake na Diamond.

“Bado hatujakutana na wala hatujawahi kukaa kuzungumzia kuhusiana na collabo.”

Msikilize Jaydee hapo chini.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW