Burudani

Lady Jaydee ataja siku ya kuachia ngoma yake mpya, imetayarishwa na mpenzi wake Spicy

Mambo yanazidi kuwa moto kwa Lady Jaydee. Malkia huyo wa Bongo Flava ametangaza ujio wa ngoma yake mpya ikiwa imepita miezi mitano tangu alipoachia wimbo wake wa mwisho uitwao ‘I Miss You’.

Jaydee ametangaza kuachia wimbo wake huo mpya March 23 ya mwaka huu na tayari ameupa jina la ‘Anaweza’ ambao amemshirikisha msanii Jepther McClymont maarufu kama Luciano kutoka Jamaica.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo Bongo5 tumeipata, mtayarishaji wa ngoma hiyo ni mpenzi wake Spicy ambaye alimshirikisha Jide kwenye wimbo wa Together Remix.

Hata hivyo video ya ngoma hiyo kuna uwezekano mkubwa ikawa imeongozwa na director Justin Campos kutokana na hivi karibuni Jaydee alipost picha wakiwa pamoja na kuandika,”Ukimuona Justin Campos nafikiri unajua moja kwa moja ni nini kinafuata @_justin_campos_ 🔥🔥🔥🔥🔥🔥.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents