AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Lady Jaydee atangaza fursa kwa wabunifu wa mavazi na wanamitindo

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Lady Jaydee ametangaza fursa kwa wanamitindo na wabunifu wa mavazi hapa Tanzania, ambao atawatumia kwenye video yake mpya.

Lady Jaydee

Lady Jaydee kupitia ukurasa wake wa Instagram, amesema kuanzia leo na kesho ataanza kupokea maombi ya watu watakaoomba kufanya naye kazi.

Nita shoot video yangu ya kwanza kwa mwaka 2019 nchini Afrika ya Kusini siku ya Alhamis 10th January 2019. Nakaribisha Stylists wapya wa nguo, Jewelry, Viatu n.k kwa siku ya leo na kesho tu,” ameandika Lady Jaydee

Lady Jaydee ametaja pia masharti ya waombaji watakaojitokeza “Unaweza kuniandikia email na kutuma picha ya vitu unavyotaka vionekane, au kutuma kwa WhatsApp kwenye number iliyopo kwenye profile yangu. Zingatia uafrika zaidi katika designs utakazotuma na u modern kidogo ukiwemo sio mbaya“.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW