Burudani

Lady Jaydee awatahadharisha mashabiki wake

Lady Jaydee amewatahadharisha mashabiki wake kutowaamini watu wanaotumia jina lake kuuza biashara zao mitandaoni.

Kupitia mtandao wa Facebook imefunguliwa akaunti ambayo inatumia jina la msanii huyo ambapo pia baadhi ya watu wamewahi kutapeliwa kupitia akaunti hiyo.

Kupitia mtandao wa Instagram Jide ameandika:

Jihadharini na ma tapeli , hii page sio yangu na inatumika kudanganya watu huko Facebook.
Kuweni makini sana
Imewahi kutokea hivi watu wakatapeliwa pesa zao na wakaja kunilalamikia. Page zangu zote ziko verified zina blue tick

Wezi wa mtandaoni wameonekana kutembea karibu na wasanii ikiwa ni muda mfupi umepita tangu msanii Beka Flavour wa Yamoto Band, alipokamatwa na polisi kwa kudaiwa jina lake kutumika kutapeli shilingi milioni tisa kupitia mtandao wa Facebook.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents