Lady Jay Dee

Lady Jaydee, Mwana FA, Izzo B na wasanii wengine waahirisha show zao kwa heshima ya Albert Mangwea

Takriban masaa 17 toka habari za msiba wa mwana chemba, Albert Mangwea aliyefariki jana (May 28) huko Africa Kusini kusambaa, tayari wadau wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya wamechukua hatua za kumpa heshima marehemu kwa kuahirisha shughuli za kiburudani zilizokuwa zifanyike weekend hii.

l-600x400

Kati ya show kubwa zilizokuwa zifanyike weekend hii ni pamoja na show ya “The Finest” ya Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA ambaye ametangaza kuahirisha show hiyo na kuisogeza hadi June 14 kama mazishi yatakuwa tayari yamefanyika. “Sina uhakika,but I’ll pick June 14th kama brother tutakuwa tushampumzisha,” ametweet.

Show nyingine kubwa iliyoahirishwa ni ya “Miaka 13 Ya Lady Jaydee” ambayo sasa haitafanyika tena (May 31). Lady Jaydee alikuwa akizungumza asubuhi ya leo kupitia kipindi cha Power Jams cha East Africa na kusema haitafanyika mpaka pale watakapotoa taarifa zaidi.

Show zingine zilizokuwa zifanyike weekend hii ni pamoja na ya Kikosi cha Mizinga wakiongozwa na Kalapina ambayo nayo haitafanyika tena kama ilivyokuwa imetangazwa hapo awali.

Naye Khalid Mohamed a.k.a TID jana kupitia akaunti yake ya facebook alielezea maamuzi yake ya kuahirisha show yake aliyokuwa aifanye Maisha Club jana usiku (May 28) pamoja na show alizokuwa afanye Bukoba weekend hii.

Mwana hip hop Izzo Business aliyetarajia kufanya show weekend hii mkoani Mbeya alitweet juu ya mabadiliko yaliyotokana na msiba huu. “Naomba radhi kwa wote waliosubiria show yangu tar 31 / 5 / 2013 The vibe nimehairisha show kutokana na msiba wa ngwea taarifa zaidi zitatoka,” alitweet jana usiku.

Ukiachilia mbali wasanii ambao wameahirisha kufanya show zao kupisha msiba huu mkubwa kwa tasnia ya muziki wa kizazi kipya Tanzania, wapo wasanii wengine ambao walipanga kutoa nyimbo pamoja na videos wiki hii.

Ben Pol ni kati ya wasanii hao ambaye alikuwa anatarajia kuachia rasmi video ya wimbo wake mpya wa Jikubali (June 1). “Sidhani kama ninayo raha ya kutoa video yangu mpya wiki hii, naomba radhi, nitapisha shughuli za mazishi ya ndugu yangu #restInPeace Albert ametangaza kuahirisha kutoa video hiyo,” aliandika.

Naye rapper wa kampuni ya Weusi John Simon a.k.a Joh Makini ameahirisha kutoa wimbo wake mpya aliopanga kutoa alhamis (May 30) na sasa haitatoka mpaka pale atakapotoa tarehe mpya. Joh alitegemea pia kufanya show club 77 ambayo ameisogeza mbele. Alitweet “Kutokana na msiba huu mzito nimesogeza mbele kuachia ngoma yangu mpya pamoja na show yangu club 71 tegeta mpaka nitakapowatangazia tena.”

RIP ALBERT MANGWEA.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents