Burudani

Lady Jaydee na Mwana FA wakutana tena studio

Baada ya kurejesha ushikaji wao hivi karibuni ambao ulipotea kwa muda, hatimaye Mwana FA na Lady Jaydee wamerudi studio kufanya kazi.

October 3 mwaka huu Mwana FA kupitia mtandao wake wa Instagram aliposti video ya wimbo mpya wa Lady Jaydee ‘I Miss You’ kitu kilicholeta shauka kwa mashabiki wa pande zote mbili kutaka kujua baada ya ushakaji huo kurudi iwapo watafanya tena kazi.

Sasa leo November 16, 2016 Lady Jadee ameposti picha katika ukurasa wake wa Instagram akiwa studio za B Hit’s na Mwana FA na kuandika; Last night 🎼🎸🎹🎤🎻🎺🥁 #Muziki, bila shaka kuna kazi ya pamoja inakuja.

Lady Jaydee na Mwana FA wameshaweza kutoa hit songs kama Hawajui, Msiache Kuongea, Alikufa kwa Ngoma na Wanaume Kama Mabinti bila kusahau ngoma walioshirikishwa na Ngwea ‘Sikiliza’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents