Burudani

Laiza kutoka nje ya box Wasafi Records

Producer kutokea Wasafi Records, Laiza amesema msanii yeyote anaweza kufanya kazi ndani ya studio hiyo na si wale wa WCB pekee.

Laiza amesema kuwa licha ya kufanya kazi na wasanii wa WCB hivi karibuni zitaanza kusikika kazi za wasanii wengine nje ya label hiyo.

“Kazi tofauti na wasanii wa WCB zinakuja, zitatoka soon,” Laiza ameiambia Bongo5.

“Nachoweza kusema wasanii tofauti wafikie studio tunawakaribisha, studio inapokea kila msanii. Kila aina ya msanii kutoka nchi tofauti, wasidhani kuwa ni Wasafi pekee,” amesema.

Dully Sykes, Chege na Madee ni miongoni mwa wasanii walionje ya WCB kufanya kazi na Laiza ndani ya Wasafi Recors. Producer huyo kwa mwaka huu anajivunia hit kama Kwa Ngwaru ya Hamornize akishirikiana na Diamond ambayo imefikisha views Milioni 10 katika mtandano wa YouTube kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents