Burudani

Lamar afunguka Bongo Flava kupungukiwa albamu, kukosa tuzo

Producer wa muziki Bongo kutoka Fish Crab, Lamah amezungumzia muziki wa Bongo Flava kupungikiwa albamu pamoja na kukosa tuzo.

Katika mahojiano na Bongo5 Lamar amesema kukosekana kwa tuzo kunaweza kupunguza ushindani miongoni mwa wasanii na albamu ni kipimo kwa msanii kujua uwezo wake wa kuchanganya ladha hivyo vitu hivi viwili kukosekana game linapwaya.

“Tuzo zina umuhimu wake kwa sababu tuzo unapopata inakuhamasisha kufanya vizuri na zaidi au kufanya ushindani na wenzako kwa hiyo inapokosekana tuzo game inakuwa kawaida kwamba hamna ushindani tena, kwa hiyo tuzo ina umuhimu wake,” “amesema Lamar.

“Albamu pia ina umuhimu wake kwa sababu  inakupa kipimo cha wewe msanii kuweza kufanya ladha tofauti kwenye albamu yako, kama utafanya RnB, hip hop, Bongo Flava, Jazz  kwa hiyo kwenye albamu utaweka nyimbo nane ambazo zitazokuwa tofauti tofauti, utaondoka utafanya featuring na msani fulani, kwa hiyo albamu ina umuhimu wake” amemaliza kwa kueleza.

Katika hatua nyingine amesema ukimya wake katika game si kwamba harekodi nyimbo bali kazi zinafanyika ila  hazijatoka kutokana na ratiba au utaratibu wa msanii husika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents