Burudani

Lamar ataja vitu alivyojifunza kutoka kwa P-Funk, marehemu Roy na Dunga katika utayarishaji muziki

P-Funk Majani, marehemu Roy na Dunga ni watayarishaji wa muziki wenye mchango mkubwa kwa producer wa Fishcrab, Lamar.

11199613_916004298456828_356042720_n

Akiongea kwenye kipindi cha Chill na Sky, Lamar alisema alianza kwenda kwa marehemu Roy ambako alijifunza jinsi ya kukata samples mbalimbali.

“Kwa marehemu Roy nimejifunza kuchop snares na kicks, samples zile na kutengeneza sound yangu mwenyewe,” amesema.

Amesema kwa Majani alijifunza zaidi masuala ya sauti.

“P-Funk amenifundisha kumix na kufanya mastering. Nilienda kwa P-Funk natengeneza beats lakini sina sikio la kumix, kwahiyo akanitrain sikio langu niweze kusikia vizuri na jinsi ya kumix na kufanya muziki uwe product sasa, sio kuwa beat maker niwe producer ambaye anaweza kumix na kumaster muziki wake na kuweza kuupeleka kwenye level ya kimataifa,” ameeleza Lamar.

Anasema alijifunza vitu vingi zaidi kwa Dunga.

“Nilijifunza kutumia software ya Logic, nimejifunza kutengeneza muziki wa aina tofauti. Ukienda kwenye salsa nipo, ukienda kwenye rnb nipo, kutokana na zile chords anazocheza na arrangement.”

Msikilize Lamar kwenye kipindi cha Chill na Sky hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents