Michezo

Lamar Odom apata fahamu baada ya tatu

Mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu katika ligi ya NBA nchini Marekani, Lamar Odom amepata fahamu baada ya hivi karibuni kupatikana akitokwa na damu puani na mdomoni na kupoteza fahamu kutokana na kutumia kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya.

Lamar Odom

Taarifa zimedai kuwa Odom alizungumza na kunyoosha kidole akiwa kwenye kitanda chake cha hospitali alikolazwa. Alikuwa akitumia mashine maalum ya kumsaidia kuishi.

151014164802_sp_lamar_odom_and_khloe_kardashian_624x351_reuters_nocredit

Wafanyakazi wa danguro la Love Ranch la huko Crystal, Nevada walisema kuwa Odom alikuwa katika danguro hilo kwa siku kadhaa na amekuwa akitumia dawa za kulevya aina ya cocaine pamoja na zile za kuongeza hamu ya kufanya mapenzi.

Odom ambaye ni mume wa zamani wa Khloe Kardashian, aliwahi kushinda taji la ubingwa akiichezea timu ya Los Angeles Lakers.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents