Burudani

Lamar Odom atolewa kwenye hospitali ya Las Vegas, apelekwa Los Angeles

Mchezaji wa kikapu wa NBA, Lamar Odom amewasili jijini Los Angeles Jumatatu usiku akiwa na mke wake wa zamani, Khloe Kardashian baada ya kusafirishwa kwa helicopter kutoka kwenye hospitali ya Sunrise ya jijini Las Vegas.

la_50greats_17

Staa huyo wa NBA atakuwa akipokea matibabu jijini L.A. baada ya Jumanne iliyopita kupatikana akiwa hajitambui kwenye danguro huko Nevada. Alidaiwa kutumia kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya na dawa za kuongeza nguvu za kiume, Viagra.

Kwa sasa afya yake imeanza kuimarika kiasi hapo vyanzo vinadai kuwa ana safari ndefu ya kuja kupona kabisa. Kabla ya kufumbua macho yake na kuongea. Lamar alikuwa hajitambui kwa takriban siku tatu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents