Michezo

Lampard na Terry nje ya England Squad

 

Kocha wa timu ya Taifa ya England Fabio Kapello, atawakosa nyota wa wawili wa Chelsea, Frank Lampard na John Terry katika mechi za kuwania kufuzu kwa fainali za Euro 2012 dhidi ya Bulgaria na Uswiss baada ya wote kuumia wakati klbu ya ikiikung’uta Stoke City Jumamosi iliyopita.

Kiungo Lampard aliachwa kwasababu ya ngiri na atalazimika kufanyiwa upasuaji mdogo wiki ijayo wakati Terry hatakuwepo kwenye kikosi cha England kutokana na msuli wa paja kupata jeraha.

Lampard alitolewa wakati wakishinda mabao 2-0 dhidi ya Stoke City huku akikosa penalty katika kipindi cha kwanza.Mchezaji huyo atafanyiwa upasuaji wiki hii,kati ya Jumanne au Jumatano hivyo hataichezea England,kocha wa Chelsea Carlo Ancelotti aliwaambia waandishi wa habari.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents