Burudani

Langa aujutia uteja

Langa_Kileo
MWANAMUZIKI wa muziki wa kizazi kipya Langa Kileo, amesema kwa sasa ameachana na utumiaji wa madawa ya kulevya aina ya Kokein, kwakuwa maisha hayo kwake aliyaona kama vile ni kifungo.

 

 

Akiongea na Bongo5, amesema ana mengi ya kuwaambia wasanii wenzake  na wananchi wote wanaotumia madawa ya kulevya waachane nayo kwakuwa yanarostisha maisha yao.

Pia mwanamuziki huyo ambaye alitamba kwa wimbo wa Matawi ya juu, alisema anawaomba msamaha wale wote ambao aliwafanyia vitendo visivyo vya kiungwana, kama vile kuwakaba na kuwaibia, kwakuwa alifanya hivyo si kwa hiyari yake.

Anasema anajutia matendo mengi ya uovu aliyoyafanya,lakini hali ya uarosto ndiyo iliyompelekea kufanya vitendo hivyo. aidha amedai hari hiyo ambayo ilikuwa kama ugonjwa ndiyo iliyokuwa ikimpelekea kuhitaji madawa ya kulevya, na hatmaye akajikuta akihama kwao kwaajili ya kuishi mtaani kwa kazi ya wizi, kupiga debe na kukaba huku akiishi kama teja.

“Hivi sasa nahitaji kuwa mwanaharakati wa kweli katika kupambana na madwa ya kulevya, naomba ushirikiano wenu wananchi”

langa

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents