BurudaniVideos

Larry Madowo: Nilipanga kuwa Padre kabla ya kuamua kuwa mtangazaji wa TV

Katika fani ya utangazaji wa TV nchini Kenya, ikiwa Larry Madowo hayupo kwenye list yako ya tano bora basi jua kwamba hamna ubora tena kwenye list yenyewe.

Madowo ni miongoni mwa watangazaji wanaofagiliwa sana pande za Kenya kwa sababu ya uwezo na ubora wake katika kila anachokifanya ndani na pia nje ya taifa.

Kando na kwamba aliwahi kufanya kazi kwenye benki kabla ya kuingia katika media, hakijatosha. Kuna kitu kingine ambacho wengi walikuwa hawakijui kumhusu jamaa huyu.

Kupitia show yake ya ‘The Trend’, mtangazaji huyu alijikuta akifanyiwa interview na muigizaji maarufu wa tamthilia ya ‘Game of Thrones’ Nikolaj Coster-Waldau anayejulikana kwa jina la Ser Jaime Lannister kwenye tamthilia hiyo aliyekuwa mgeni wake.

Muigizaji huyo maarufu kutoka Marekani alimuuliza Larry kuhusu kitu Wakenya na wafuasi wake kwa ujumla hawakijui kumhusu. Aliweka wazi kwamba alitaka sana kuwa Padre lakini alikomea njiani.

“I really wanted to be a priest but I dropped out after 4 years of training.”

Aliendelea na kusema kwamba kilichomzuia kuendelea ni vitu fulani ambavyo asingeweza kufanya kama kuwa kufunga ndoa na kuwa na familia yake. Hii hapa kwa kweli wengi hawakuijua kumhusu mtangazaji huyu maarufu.

Imeandikwa na : Teddyza Agwa
Instagram @teddybway

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents