Lava lava afunguka ishu ya wasanii wa WCB kuvaa cheni zenye ‘misalaba’

Mwaka jana kulikuwa na stori nyingi mtandaoni kuhusu Wasanii wa WCB kuvaa mikufu yenye misalaba shingoni kitu ambacho baadhi ya watu wamekuwa wakihusisha na imani tofauti tofauti huku baadhi ya waislamu wakidai kuwa hiyo ni ishara ya kukubaliana na dini ya Kikristo.

Sasa msanii wa Bongo Fleva kutoka WCB, Lava Lava amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ishu hiyo ya kuvaa cheni hizo zenye misalaba akidai kuwa ni Swaga tu hakuna jambo lingine nyuma ya misalaba hiyo huku akikana kuwa ile siyo misalaba kama inayotumiwa na Wakristo makanisani.

Mimi sijawahai kuona msalaba ambao una duara kwa juu, sijawahi kuona, ama msalaba huwa unakuwa hivyo?, mimi sijui labda kama kuna mkristo atusaidie alama ya msalaba huwa inakuwa vipi?“amesema Lava Lava kwenye kipindi cha Playlist cha Times Fm na kuelezea sababu ya WCB kuvaa cheni zenye misalaba,”Mimi sijavaa msalaba ile mimi naona ni swaga tu, yaani ni swaga tu hakuna ishu“.

Tukio la Wasanii wa WCB akiwemo kiongozi wao Diamond Platnumz la kuvaa cheni zenye misalaba mwishoni mwa mwaka jana (2017) liliibua hisia tofauti tofauti kwa waumini wa dini ya Kiislamu wakiwepo mashekhe waliokuwa wanahoji kuwa muislamu halisi hawezi kuvaa msalaba wala kutamka neno ‘Hallelujah’ kama Diamond alivyofanya kwenye wimbo wake wa Hallelujah.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW