Burudani

Lavalava aweka wazi mahusiano yake na Irene Uwoya ” Akipika chai utafikiri amepika biriani ” – Video

"Mimi namcrush sana Uwoya ni mwanamke aliyekamilika kila idara ana tabia nzuri sana anafaa kua Wife Material akipika chai utafikiri kapika biriani"

Msanii wa muziki wa bongo fleva Lavalava ambaye yuko chini ya lebo ya muziki ya WCB ambayo inasimamiwa na Diamond Platnumz, amefunguka kuhusu mahusiano yake na msanii wa bongo movie Irene Uwoya.

Akiongea kwenye kipindi cha The playlist kinachoruka Times fm Lavalava amesema kuwa yeye na Irene Uwoya ukaribu wao hauna maana nyingine tofauti na ushkaji japo Uwoya ni mwanadada mrembo anayemvutia kila mwanaume.

“Uwoya ni mwanamke ambaye anamvutia mwanaume yeyote yule lakini Mimi na yeye ni washkaji tu hakuna kingine,nashangaa hizi story sijui zimeanzia wapi”

Lavalava alipoulizwa ni msanii gani wa kike anaemvutia kimapenzi amesema anavutiwa na Uwoya na ni mwanamke ambaye anatamani kua nae kimahusiano

“Mimi namcrush sana Uwoya ni mwanamke aliyekamilika kila idara ana tabia nzuri sana anafaa kua Wife Material akipika chai utafikiri kapika biriani”

By Angel Mmasi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents