Burudani

Lebo ya Kaka Empire ya King Kaka yamsaini producer tishio Kenya

By  | 

Lebo maarufu ya muziki nchini Kenya, Kaka Empire inayomilikiwa na King Kaka imemsaini mtayarishaji wa muziki maarufu nchini humo, Jack Jack On The Beat.

Mmoja wa viongozi wa lebo hiyo, ameiambia Bongo5, Jack atakuwa ndio mtayarishaji mkuu katika studio ya Kaka Empire Studios.

Naye mtayarishaji huyo baada ya kusaini mkataba huo amesema, “Kujiunga na Kaka Empire ni uamuzi bora zaidi ambao nimeufanya mwaka huu. Wakati fulani katika maisha mtu unatakiwa kujiunga na timu ya kushinda.”

Jack ameshawahi kutayarisha ngoma kibao kali ikiwemo Tippy Toe, Bazokizo, Zigwembe, Sema Ng’we na nyingine.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments