Burudani

Lengo langu ni kuwa director bora duniani – Hanscana

By  | 

Muongozaji wa video za muziki nchini, Hanscana amedai kwa sasa yupo kwenye kipindi cha kutengeneza kazi nyingi na bora ambazo zitamfanya akubalike dunia nzima.

Hanscana akiwa mzigoni

Hanscana ambaye ameongoza video mpya ya wimbo ‘Ukivaaje Unapendeza?’ ya rapa Dogo Janja kutoka Tip Top Connection, ameiambia Bongo5 kuwa  kwa sasa anahakikisha anafanya video nyingi zenye ubora wa kimataifa ili kuweza kuwavuta wateja wa kimataifa.

“Kwa sasa nipo kwenye kipindi cha mpito cha kutengeneza kazi nzuri ambazo zitakubalika na dunia nzima. Nadhani kwa East Afrika tunanya vizuri na bado tunaendelea kutengeneza kazi nyingi bora ambazo zitanifanya kuwa director bora duniani,” alisema Hanscana.

Aliongeza, “Kama unavyoona sasa hivi hapa nchini nafanya kazi nyingi sana na wasanii wakubwa, ukiangalia kazi nilizofanya mwaka jana hauwezi kuzilinganisha na kazi za mwaka huu, kwahiyo mimi sina chakusema zaidi ya kuwaahidi mashabiki wangu wasubirie kazi nzuri zaidi zenye ubora wa kimataifa,”

Muongozaji huyo kwa sasa ni mmoja kati ya waongozaji wa video za muziki nchini anayefanya kazi nyingi na wasanii wa hapa nchini.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments