Michezo

Lengo letu Yanga ni kutetea ubingwa – Nadir Haroub ‘Cannavaro’

Nahodha wa klabu ya Yanga, Nadir Horoub ‘Cannavaro’ amesema kwa sasa klabu yake inajiandaa msimu ujao kutwaa taji la nne mfululizo la Ligi kuu Tanzania bara na kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.

Cannavaro amesema kipindi hiki cha mapumziko wanafanya mazoezi ya kujiweka vizuri kwa ajili ya mikiki mikiki ya msimu ujao ambao unaonekana kuwa msimu mgumu kuliko yote kutokana na uwekezaji uliofanywa na kampuni ya kubashiri ya Sportpesa kwenye vilabu vinavyoshiriki ligi kuu.

“Lengo letu la kwanza ni kutetea ubingwa mara nne mfululizo hilo ndiyo lengo la kwanza lengo la pili ni kuweza kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa”,amesema Cannavaro kwenye mahojiano yake na SportPesa.

Hata hivyo Cannavaro ameipongeza Kampuni ya SportPesa kwa udhamini wake ndani ya Klabu ya Yanga kwa kusema kuwa wameongeza molali kwa mchezaji mmoja mmoja na kuisaidia timu yake kuona njia ya kufika wanapopataka.

Klabu ya Yanga imepiga kambi mkoani Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2017/18 unaotarajiwa kuanza mwezi Agosti mwaka huu.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents