Burudani

Leo Harmorapa sijui ana kitu gani kipya – Timbulo

Msanii wa Bongo Flava, Timbulo amesema ni vema wasanii kutengeneza mazingira ya watu kupenda muziki wao na si vitu vingine ambavyo visipokuwepo na muziki wao unashuka.

Muimbaji huyo amesema kutokana na baadhi ya wasanii kutengeneza matukio hayo ‘kiki’, inafika wakati watu wanalinganisha wasanii wasio na uwezo sawa kisa mmoja wapo amebebwa na kiki.

“Leo Harmorapa sijui ana kitu gani kipya anaweza kufanya, mimi nilimsapoti mwanzo alichokuwa anafanya, nikasema yupo sawa kwa mtazamo wake, na ndio aina yake ya maisha ambayo ameyachagua, lakini je itamsaidia kwa kipindi kirefu?,” alihoji Timbulo na kuendelea.

“Watu wanakuja wanapenda vurugu kesho ukiacha vurugu ukafanya muziki unajikuta na watu 10 katika 100 wanaopenda muziki wako, ina maana watu 90 wote wameondoka,” amesema Timbulo.

Katika hatua nyingine msanii huyo ametaja sababu ya kufanya maisha yake ya kimahusiano kuwa siri, “let say, leo natembea na Wema, kesho tukiachana walionipenda kwa sababu yake watakuwa maadui zangu,” ameiambia Radio One na kuongeza.

“Kwa hiyo ukiweka maisha yako private mtu akija kwako ni kwa sababu ya muziki wako tu ingawa itachukua time lakini kila siku ukitoa kazi utaongeza watu wapya japokuwa unaweza kuwa hauoni,” amesema Timbulo.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents