Habari

Leo ni miaka saba tangu kifo cha Vivian na Complex…Tunazidi kuwakumbuka

Ilikuwa ni siku ya Jumapili ya tarehe 21 August mwaka 2005 majira ya saa tatu asubuhi siku ambayo nyota wawili wa muziki nchini waliokuwa wakipendwa sana, producer na rapper Saimon Sayi aka Complex ambaye kipindi hicho alikuwa akifanya kazi na studio ya Aigies Records na mtangazaji wa Clouds FM na rapper Vivian Tillya walifariki kwa ajali ya gari eneo la Mbwewe.
Wasanii hao ambao walikuwa wapenzi walikuwa safarini kutoka Morogoro kwenye Fiesta iliyokuwa imepewa jina la ‘Moto Zaidi’ ambapo walikuwa wanaelekea jijini Arusha kwenye Anniversary ya ndoa ya miaka 25 ya ndoa ya wazazi wake na Vivian.
Siku hiyo pia Vivian alikuwa anaenda kumtabulisha Complex kama mchumba wake kwa wazazi wake lakini mauti ikawakatisha.
Mdogo wake Vivian ambaye wakati huo alikuwa anasoma kidato cha tano Irene Tillya ambaye naye ni mtangazaji wa radio ya mtandao, Tone Radio ya jijini Dar es Salaam, ameandika kupitia Facebook, “Our roots say we’re sisters, our hearts say we’re friends. It’s now 7 years since you left us… u will always be part of me.. I love you. May your sweet soul continue to rest in peace. I miss you sis.”
“Even though we spend little time together but we are family. Miss you shemeji. It’s now 7 years since you left us. May your good soul continue to rest in peace. I hope you people are happy there. Miss u.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents