Michezo

Leo ni siku ya kuzaliwa kwa mkali wa mabao,Didier Drogba

Kwenye mpira maisha kwa wachezaji huwa mazuri kipindi ambacho timu yake inafanya vizuri na yeye anapong’aa kwa kufungia timu yake mabao mengi.

didierdrogba

Leo ni siku muhimu ya kuzaliwa kwa aliyekuwa mchezaji wa timu ya Chelsea, Didier Drogba ambaye ni mmoja kati ya wachezaji wa kiafrika wasioweza kusahaulika kwenye timu hiyo.

Drogba aliweza kuisaidia timu ya Chelsea kuchukua makombe kibao, EPL(2), FA(1), na UEFA (1) . Timu alizowahi kuchezea mchezaji huyo ni, Le Mans, Guingamp, Marseille, Chelsea, Shaghai, Galatasaray, na sasa anachezea timu ya Montreal Impact inayoshiriki ligi kuu ya nchini Marekani.

Drogba alizaliwa Machi 11, 1978 huko Abidjan, nchini Ivory Coast. Mpaka sasa Drogba ameshafunga jumla ya magoli 275 tangu aanze kucheza mpira wa kulipwa.

Happy Birthday Didier Drogba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents